Inosenti wa Tortona

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Inosenti wa Tortona (Tortona, Italia Kaskazini, 285 - Tortona 17 Aprili 353) anakumbukwa kama askofu wa mji huo.

Ujanani alidhulumiwa kwa ajili ya imani ya Kikristo katika dhuluma ya kaisari Dioklesyano (303).

Mwaka 313 alihamia Roma alipofanywa na Papa Silvesta I kuwa shemasi na hatimaye askofu wa mji wake asili, alipoimarisha jimbo na kupambana na Upagani[1].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu[2].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 17 Aprili[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/91520
  2. Flavio Peloso, "San Marziano e sant'Innocenzo. Don Orione cultore delle origini cristiane di Tortona Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.", in Iulia Dertona. Bollettino della Società storica tortonese per gli studi di storia, d'economia e d'arte (convegno, Tortona 15 maggio 2013).
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.