Innoss'B

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Innoss B akitumbuiza.

Innocent Didace Balume (anajulikana sana kwa jina la Innoss'B; alizaliwa 5 Mei 1997) ni mwanamuziki na mwandishi wa nyimbo kutoka katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ni mwanamuziki mzuri mwenye uwezo wa kucheza na kurapu.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Innoss'B alizaliwa kwenye familia ya wanamuziki, mama yake alikuwa mwimbaji wa kanisa, baba yake alikuwa mwanamuziki wa popu. Na yeye, baada ya kufikisha miaka 16, alianza kuimba na kaka zake kwenye kundi la Maisha Soul.

Tangu mwaka 2014 amefanya kolabo nyingi na wasanii wakubwa mbalimbali kama Akon, Fally Ipupa, Diamond Platnumz, Navio na wengineo.

Amepata mafanikio makubwa kupitia hope remix ambayo amefanya na Diamond Platnumz ambayo iliweza kufikisha watazamaji milioni 25 ndani ya mwezi mmoja ambayo imezidi hope original ambayo ilifikisha watazamaji milioni 10 tu ndani ya mwezi mmoja.

Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Innoss'B kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.