Igamba (Dodoma)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Igamba ni jina la kijiji kilichopo katika kata ya Dabalo, wilaya ya Dodoma vijijini.

Mradi wa umeme wa TANESCO umeingia mwaka 2013 na mwaka huo viongozi waliwaahidia wanakijiji wa Igamba kuwa umeme utawaka miaka ya hivi karibuni.

Mnamo Septemba 2013 wakaja wafanyakazi wa Tanesco na kupima sehemu zinazohitaji kuchimbia nguzo za umeme na kuweka vigingi.

Mnamo Februari 2014 likaja lori aina ya SCANIA na kushusha nguzo kijijini Igamba.

Kijiji cha Igamba kilikuwa hakina maendeleo lakini sasa ni moto wa kuota mbali, pia kilikuwa hakina mawasiliano ya kutumia simu za mkononi: ilikuwa hadi mtu apande juu ya mti, tena baadhi ya sehemu, lakini sasa wanakijiji wa Igamba wanatumia mawasiliano ya Halotel (Viettel).