Nenda kwa yaliyomo

Dabalo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dabalo ni kata ya Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania, yenye postikodi namba 41409[1].

Kata hiyo ina vijiji kama vile Dabalo, Membe, Mtungu Chole, Mkadaji, Ikombo na Silale.[2]

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 26,241 [3]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 16,115 [4] waishio humo.

Wenyeji wa kata hii wengi wao ni Wagogo ambao huendeleza shughuli za sanaa za tamaduni zao kama vile sanaa ya kuimba, kucheza na kuchora. Hivyo Dabalo hufanyika mambo mengi ya kisanaa, kama wacheza filamu, wasanii chipukizi wa muziki wanaofanya vizuri.

Wamasai, Wairaqw na Wanguu pia wanapatikana kwa wingi katika kata hiyo yenye ardhi kubwa na yenye rutuba. Watu hao wote wameingia hapo miaka mingi hata wana vizazi vingi kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji, mbali na uvuvi na biashara ambazo pia hukuza uchumi wa kata hiyo.

Mazao ambayo hulima ni pamoja na karanga, mahindi, alizeti, maharage, mbaazi na kilimo kidogo cha umwagiliaji kutokana na bwawa la Dabalo ambalo linaleta maendeleo asilimia 40 kwa kila mwaka na linavutia wageni wengi kuitembelea Dabalo mara kwa mara..

Ng'ombe, mbuzi na kondoo ni kati ya mifugo ambayo wenyeji wa kata hiyo hufuga kwa ajili ya uchumi wao. Punda hufugwa kwa asilimia chache kwa ajili ya kubeba mizigo kwa shughuli mbalimbali.

  1. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-03-21. Iliwekwa mnamo 2017-10-08.
  2. "Gmail". accounts.google.com. Iliwekwa mnamo 2024-12-26.
  3. https://www.nbs.go.tz
  4. "Sensa ya 2012, Dodoma - Chamwino DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-18.
Kata za Wilaya ya Chamwino - Mkoa wa Dodoma - Tanzania

Buigiri | Chamwino mjini | Chiboli | Chilonwa | Chinugulu | Dabalo | Fufu | Handali | Haneti | Huzi | Idifu | Igandu | Ikombolinga | Ikowa | Iringa Mvumi | Itiso | Loje | Majeleko | Makang'wa | Manchali | Manda | Manzase | Membe | Mlowa Barabarani | Mlowa Bwawani | Mpwayungu | Msamalo | Msanga | Muungano | Mvumi Makulu | Mvumi Misheni | Nghahelezi | Nghambaku | Nhinhi | Segala | Zajilwa


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Dabalo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.