I Need a Beat ni single ya kwanza kutoka kwa rapa, LL Cool J, na ni moja kati ya matoleo mawili ya Def Jam Recordings kuwa na nembo katalogi ya namba, sambamba kabisa na Beastie Boys' "Rock Hard". Ilitolewa mnamo mwaka wa 1984 kwa ajili ya Def Jam Recordings, imetayarishwa na Rick Rubin na kutungwa na Rubin, LL Cool J na Adam Horovitz wa Beastie Boys. Baadaye wimbo ulirudiwa tena na kutumbukizwa kwenye albamu yake ya kwanza ya Radio.