Ain't Nobody
“Ain't Nobody” | ||
---|---|---|
Single ya Rufus & Chaka Khan kutoka katika albamu ya Stompin' at the Savoy | ||
Imetolewa | 4 Novemba 1983 | |
Imerekodiwa | 1982-1983 | |
Aina | Pop/Soul/R&B | |
Urefu | 4:41 | |
Studio | Warner Bros | |
Mtunzi | Hawk Wolinski |
"Ain't Nobody" ni kibao kikali cha mwaka wa 1983 ambacho kiliimbwa na kundi zima la Rufus & Chaka Khan. Kilitolewa kikiwa kama wimbo wa ziada katika albamu yao moja-kwa-moja ya bendi Stompin' at the Savoy. Kibao hiki kilifikia nafasi ya kwanza katika chati za miondoko ya R&B huko nchini Marekani na kushika nafasi ya ishirini-na-mbili katika chati za Billboard Hot 100.[1] Kibao hiki kimepata kuwa moja kati ya alama maarufu ya nyimbo za Khan.
Mpiga kinanda wa Rufus David "Hawk" Wolinski ametunga kibao hiki kwa kutumia synthesizer inayojirudia yenyewe kwa mashine ya ngoma ya LinnDrum. Mtayarishaji mkongwe Quincy Jones (ambaye awali alifanyakazi na kina Rufus) alimtaka Wolinski autoe wimbo wa "Ain't Nobody" kwa Michael Jackson kwa ajili ya albamu iliyotingisha dunia, Thriller, lakini kwa bahati mbaya Wolinski tayari alikuwa ameahidi kurekodi kibao hiki kwa Russ Titelman, ambaye hatimaye amekifanya kuwa kibao cha kundi kwa kuimbwa na Khan.
Wimbo huu pia ulijumlishwa katika orodha ya vibwagizo vya filamu ya Breakin'.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Whitburn, Joel (2004). Top R&B/Hip-Hop Singles: 1942-2004. Record Research. uk. 505.
- ↑ Breakin'