Nenda kwa yaliyomo

Homa ya mgunda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Homa ya mgunda
Leptospirosis - Homa ya mgunda
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuInfectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10A27.
ICD-9100
OMIM607948
DiseasesDB7403
MedlinePlus001376
eMedicinemed/1283 emerg/856 ped/1298
MeSHC01.252.400.511

Homa ya mgunda (jina la kitaalamu: leptospirosis [1] Majina mengine ya Kiingereza ni field fever, rat catcher's yellows [2] na pretibial fever [3] miongoni mwa mengineyo) ni ugonjwa unatokana na maambukizo yasababishwayo na bakteria za Leptospira [4]. Dalili zinaweza kuenea kuanzia na kuumwa kwa kichwa, maumivu ya musuli, na homa; hadi damu kutoka mapafu au homa ya uti wa mgongo.[5][6]

Kama uambukizo unamsababishia mgonjwa kuumia homa ya manjano, kuzuia figo kutofanya kazi pamoja na kutoka kwa damu, matokeo ni maradhi yajulikanayo kama Weil's disease.[6] Kama maradhi yanasababisha damu kutoka kwa wingi mapafuni yanajulikana kama mlimbiko dalili za damu kutoka mapafuni kwa wingi (severe pulmonary haemorrhage syndrome).[6]

Chanzo na uaguaji

[hariri | hariri chanzo]

Hadi aina 13 za ukuaji tofauti za “Leptospira” zinaweza kuumiza binadamu. [7] Maradhi haya yanaambukizwa na wanyama wafugwa pamoja na wanyama porini. [6] Wanyama wa kawaida wenye kuambukiza ni( [wanyama wagugunaji mfano panya] ) [8] Mara nyingi maradhi yanaambukiza yakibebwa na ( [mkojo wa mnyama] ) au maji ama ardhi inayojaa mkojo wa mnyama kuingia kwenye ngozi ya binadamu iliyyojeruhiwa ama macho, mdomo au pua.[5][9] Kwa hiyo huhesabiwa katia ya magonjwa ya zuonosia.

Katika dunia inayoendelea maradhi kwa kawaida yanaathiri wakulima pamoja na wakaaji masikini wa miji mikubwa.[6] Katika nchi tajiri kwa kawaida watu wanaofurahia matukio ya nje nyumbani kwenye maeneo ya joto kiasi na kwenye mito na bahari ndio wanaoambukizwa. .[5] Uaguzi unafuatilia uchunguzi wa ([kiuavijasumu] )dhidi ya bakteria ama kutambulisha DNA yake katika damu. [10]

Ugangakinga na matibabu

[hariri | hariri chanzo]

Bidii zenye kuzuia maradhi haya ni pamoja na vifaa vyenye kinga kuzuia kugusana na wanyama ambao huenda wameambukizwa, halafu kunawa vizuri baada ya kazi inayowahusika wakiwa na wanyama wale. Pia kupunguza idadi ya panya katika sehemu ambako watu wanaishi na kufanya kazi.[5] . ( [Kiuavijasumu] ) kiitwacho ( [“doxycycline”] ), kinapotumika katika jitihada za kuzuia uambukizo kwenye wasafiri, hakina manufaa ambayo yamethibitishwa. .[5] Dawa za chunjo kwa wanyama zipo kwa namna fulani ya “Laptospira” ambayo pengine itapunguza hatari ya kusambaa na kuwaambukiza binadamu.[5] . Matibabu kama mtu amambukizwa ni viuavijasumu mifano ni: “doxycycline, (penisilini), au (“ceftriaxone”).[5] Maradhi ya Well yakiwa pamoja na mlimbiko dalili za damu kutoka mapafuni kwa wingi unasababisha kima za kifo zinazozidi 10% na 50% kila namna, hata kama matibabu yanapatikana. ref name=McB2005/>

Elimumaambo

[hariri | hariri chanzo]

Inakadiriwa ya kuwa watu milioni saba hadi kumi wanaambukizwa leptospirosos kila mwaka.[11] Idadi ya vifo inayosababishwa haijathibitishwa. [11] Maradhi haya yanapatikana zaidi katika mazingira ya joto jingi ya dunia lakini yanaweza kuumia kokote kule.[5] Milipuko wa maradhi haya inayosambaa upesiupesi pengine inaweza kutokea katika sehemu masikini sana za miji mikubwa ya nchi tajiri.[6] Maradhi haya yalielezwa kwa mara ya kwanza na Daktari Weil nchini Ujerumani mnamo mwaka wa 1886. Wanyama wanaoambukizwa huenda hawana dalili, ama dalili zisizo kali, au dalili kali.[7] Dalili zenyewe zinaweza kutofautisha kutokana na mnyama husika.[7] Wanyama wengine ‘ ‘Leptospira ‘ ‘ huishi katika njia ya uzazi, inayoongozea kuambukiza katika unono.[12]

  1. Mosby's Medical Dictionary (tol. la 9). Elsevier Health Sciences. 2013. uk. 697. ISBN 9780323112581.
  2. McKay, James E. (2001). Comprehensive health care for dogs. Minnetonka, MN.: Creative Pub. International. uk. 97. ISBN 9781559717830.
  3. James, William D.; Berger, Timothy G.; na wenz. (2006). Andrews' Diseases of the Skin: clinical Dermatology. Saunders Elsevier. ISBN 0-7216-2921-0. {{cite book}}: Explicit use of et al. in: |author= (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link): 290 
  4. Leptospira ni sehemu ya jamii ya spirochetes
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 5.5 5.6 5.7 Slack, A (Julai 2010). "Leptospirosis". Australian family physician. 39 (7): 495–8. PMID 20628664.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 6.2 6.3 6.4 6.5 McBride, AJ; Athanazio, DA; Reis, MG; Ko, AI (Okt 2005). "Leptospirosis". Current opinion in infectious diseases. 18 (5): 376–86. doi:10.1097/01.qco.0000178824.05715.2c. PMID 16148523.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 7.0 7.1 7.2 "Leptospirosis" (PDF). The Center for Food Security and Public Health. Oktoba 2013. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Wasiński B, Dutkiewicz J (2013). "Leptospirosis—current risk factors connected with human activity and the environment". Ann Agric Environ Med. 20 (2): 239–44. PMID 23772568.
  9. "Leptospirosis (Infection)". Centers for Disease Control and Prevention. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. Picardeau M (Januari 2013). "Diagnosis and epidemiology of leptospirosis". Médecine Et Maladies Infectieuses. 43 (1): 1–9. doi:10.1016/j.medmal.2012.11.005. PMID 23337900.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. 11.0 11.1 "Leptospirosis". NHS. 07/11/2012. Iliwekwa mnamo 14 March 2014. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help)
  12. Faine, Solly; Adler, Ben; Bolin, Carole (1999). "Clinical Leptospirosis inAnimals". Leptospira and Leptospirosis (tol. la Revised 2nd). Melbourne, Australia: MediSci. uk. 113. ISBN 0 9586326 0 X.