Historia ya Panama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Panama inahusu eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya Panama.

Baada ya ukoloni wa Hispania Panama ilikuwa sehemu ya kaskazini ya Kolombia. Majaribio mbalimbali ya uasi dhidi ya Kolombia kwa shabaha ya kuwa nchi ya pekee katika karne ya 19 hayakufaulu.

Mabadiliko makubwa yaliletwa na ujenzi wa mfereji wa Panama.

Utangulizi wake ulikuwa reli kutoka Colon upande wa Karibi kwenda mji wa Panama upande wa Pasifiki iliyojengwa mwaka 1855. Reli hii ilirahisisha safari kati ya Atlantiki na Pasifiki kwa watu na bidhaa kuelekea Kalifornia. Watu wengi walikwenda Kalifornia miaka ile kwa sababu ya dhahabu iliyopatikana kule tangu mwaka 1848 na hapakuwa na reli kati ya pwani zote mbili za Marekani wakati ule.

Colon, Panama.

Wakati wa mwisho wa karne ya 19 Marekani ilianza kujenga mfereji kati ya bahari mbili wa kukata shingo la nchi. Serikali ya Marekani iliona umuhimu wa kutawala njia hii. Ikasaidia Wapanama waliotaka kujitenga na Kolombia kwa kutuma manowari Colon iliyozuia jitihada za Kolombia za kukandamiza ghasia hiyo.

Tarehe 3 Novemba 1903 Panama ilitangaza uhuru wake na kufanya mkataba na Marekani. Panama ilikodisha mlia wa nchi kwa pande zote mbili za mfereji kwa Marekani; Marekani iliahidi kutunza uhuru wa Panama.

Hali halisi ukanda wa mfereji ilikuwa eneo la Kimarekani hadi 31 Desemba 1999 iliporudishwa kwa serikali ya Panama.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Panama kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.