Panama City

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Panama City
Nchi Panama
Casco Viejo - kitovu cha kale cha mji
Nyumba katika Casco Viejo
Kitovu kipya cha mji

Panama City (kihisp. Panamá -Mji wa Panama-) ni mji mkuu na pia mji mkubwa wa nchi ya Panama. Ina wakazi 700,000.

Mji ulianzishwa mwaka 1519 na Wahispania kwenye mahali 8 km kutoka mji wa leo. Mji wa Panama ulikua kama kituo cha usafiri kwa sababu shingo la nchi la Panama ni njia fupi ya usafiri wa barabara kati ya bahari za Pasifiki na Atlantiki. Sehemu kubwa ya fedha iliyochimbwa katika migodi ya Peru ilipitia Panama ikiwa njiani ya kupelekewa Hispania.

Mji huu wa kwanza uliharibiwa mwaka 1671 na mharamia Mwingereza Henry Morgan. Maghofu yake leo hii ni mahali pa utalii na kuitwa "Panama la Vieja" (kihisp.: Panama ya Kale).

Mji mpya ulijengwa mwaka 1673 takriban 8 km kutoka mahali pa awali. Sehemu hii inaitwa leo "Casco Viejo" (kihisp.: fuvu la kale).

Baada ya uokotaji wa dhahabu katika Kalifornia mwaka 1848 Panama ulikuwa tena kituo muhimu sana kwa sababu watu wengi walisafiri kwa meli kutoka Ulaya na pia pwani la mashariki ya Marekani kwenda Kalifornia kupitia mji wa Panama. Reli iliyojengwa 1855 kati ya bahari zote mbili iliongeza umuhimu wa mji.

Kilele chake kilikuwa ujenzi wa mfereji wa Panama kilichofanya mji kituo cha mpito kinachojulikana kote duniani.