Nenda kwa yaliyomo

Hirohito wa Japani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfalme Mkuu Hirohito, mwaka wa 1926

Hirohito (29 Aprili 19017 Januari 1989) alikuwa mfalme mkuu wa 124 (Tenno) wa Japani. Alimrithi baba yake Yoshihito tarehe 25 Desemba 1926 na kuwa mfalme hadi kifo chake. Aliyemfuata ni mwanaye Akihito.

Ingawa alijulikana sana nje ya Japan kwa jina lake la Hirohito (裕仁?) kwa Kijapani, kwa sasa anatambulika zaidi kwa jina la Shōwa.[1]

Neno Shōwa linamaanisha mtu mkarimu; ni jina la nyakati za Kijapani zilizoambatana na watawala wa nchi hiyo walioitwa Matenno wa Japani .

Maisha yake

[hariri | hariri chanzo]

Hironito alizaliwa katika ikulu ya Tokyo (wakati wa utawala wa babu yake Meiji). Baba yake aliitwa Yoshinito ambaye jina la utawala lake aliitwa Taishō) na mama yake aliitwa Sadako ambaye jina lake la utawala aliitwa Teimei.

Mwanzoni mwa utawala wake, Japan tayari ilikuwa moja kati ya mataifa yenye nguvu duniani na ilikuwa nchi ya tisa kwa maendeleo ya uchumi duniani na moja kati ya nchi nne wanachama wa kudumu wa Shirikisho la Mataifa ambalo lilikuwa shirikisho tangulizi la ya Umoja wa Mataifa.[2]

Angalia pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Northedge, Frederick S. (1986). The League of Nations: Its Life and Times, 1920–1946. New York: Holmes & Meier. ku. 42–48. ISBN 978-0841910652.
  2. Ponsonby-Fane, Richard. (1959). The Imperial House of Japan, p. 337.
Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Japani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hirohito wa Japani kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.