Hifadhi ya bahari ya Dar es Salaam
Hifadhi ya bahari ya Dar es Salaam | |
Dar es Salaam Marine Reserve System | |
Fungu Yasini reef | |
Nearest city | Dar es Salaam |
---|---|
Eneo | 15 km² |
Mamlaka ya utawala | Marine Parks & Reserves Authority (Tanzania) |
Tovuti rasmi |
Hifadhi ya bahari ya Dar es Salaam inajumlisha maeneo kadhaa kwenye Bahari Hindi karibu na Dar es Salaam, Tanzania. Kwa jumla kuna visiwa tisa visivyokaliwa na watu pamoja na sehemu za bahari kati ya visiwa hivi. Kuna visiwa vinne upande wa kusini wa Dar es Salaam ambavyo ni Bongoyo, Mbudya, Pangavini na Fungu Yasini, halafu vitano upande wa kusini ambavyo ni (Makatumbe, Finda na Kenda). Hifadhi hii inalinda sehemu za matumbawe, za miti ya mikoko na mimea mingine chini ya uso wa maji.
Utawala
[hariri | hariri chanzo]Utawala wa hifadhi ya bahari umo mikononi mwa bodi ya wadhamini wa Hifadhi na Maeneo Tengefu ya Bahari.
Maeneo tengefu ya bahari ya Dar es Salaam yalianzishwa kufuatana na sheria ya uvuvi ya mwaka 1970 [1] yakipelekwa baadaye kwa idara ya Hifadhi na Maeneo Tengefu ya Bahari [1] Ilihifadhiwa 29 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine..
Matumizi na matatizo
[hariri | hariri chanzo]Visiwa vya Bongoyo na Mbudya hasa vinatembelewa mara nyingi na watalii wageni na wazalendo pia wanaofika kwa kuogelea, kupumzika ufukoni, kutazama matumbawe au kutembea visiwani. Hata hivyo idadi kubwa ya wageni wasiosimamiwa imesababisha matatizo ndani ya maeneo tengefu.
Wavuvi wa Kunduchi, Unonio, na Msasani wanategemea samaki waliopo katika maeneo tengefu. Mashindano kati ya wavuvi pamoja na uhaba wa usimamizi yalisababisha uharibifu hasa kwa kutumia nyavu za kukamata samaki zilizo ndogo na pia mabomu yanaoharibu matumbawe pamoja na samaki changa.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Website of Marine Parks and Reserves of Tanzania Ilihifadhiwa 4 Agosti 2013 kwenye Wayback Machine.
- Imepiga Hatua Katika Kuendeleza Hifadhi na Maeneo Tengefu ya Bahari Ilihifadhiwa 28 Machi 2016 kwenye Wayback Machine. na Marko Gideon, tovuti ya ipsinternational mnamo Aprili 2012, iliangaliwa Januari 2017
![]() | Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya bahari ya Dar es Salaam kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-05-15. Iliwekwa mnamo 2017-01-23.