Heinrich Hertz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Heinrich Hertz
Picha halisi ya Heinrich Hertz.

Heinrich Rudolf Hertz (22 Februari 1857 - 1 Januari 1894) alikuwa mwanafizikia wa Ujerumani.

Mwaka 1888 aligundua mawimbi ya redio yaliyotabiriwa hapo awali na mlinganyo wa Maxwell. Pia alionyesha kwamba mwanga ni aina ya mawimbi ya umeme. Kwa heshima yake kipimo cha marudio ya mawimbi kimeitwa kwa jina lake mwenyewe: Hertz (pia Hezi, kifupi Hz).

Hertz alizaliwa huko Hamburg mwaka wa 1857. Alijifunza uhandisi huko Frankfurt na baadaye Chuo Kikuu cha Munich. Alimaliza Ph.D. yake katika Chuo Kikuu cha Berlin. Alifundisha na kuendelea utafiti katika Chuo Kikuu cha Bonn na Chuo Kikuu cha Kiel.

Alikufa kutokana na kuwemo kwa sumu mwenye damu.

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Heinrich Hertz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.