Mlinganyo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mlinganyo ni kama mizani; ni muhimu ya kwamba hatua zinatekelezwa pande zote mbili kwa shabaha ya kurahisisha mlinganyo

Mlinganyo (kutoka kitenzi "kulinga") katika hisabati (aljebra) ni kauli inayosema kuwa viwango viwili ni sawa yaani vinalingana. Milinganyo yote hutumia alama ya "="

kama vile 2 + 3 = 5

ambayo inasema "mbili ongeza tatu inalingana na tano".

Mlinganyo wa undani zaidi unatumia alama kwa viwango visivyojulikana awali na vinapaswa kugunduliwa,

Mfano :

3x + 3 = 9

Suluhisho linapatikana kwa kufuata hatua zinaopeleka "x" peke yake upande mmoja wa mlinganyo. Hatua hizi zinapaswa kuwa sawa pande zote mbili:

  • 3x + 3 - 3 = 9 -3 (ondoa 3 pande zote mbili)
  • 3x = 6
  • 3x : 3 = 6 : 3 (gawanya kwa 3 pande zote mbili)
  • x = 2

Hapo kazi ni kujua maana ya x ni nini ambayo ni 2 katika mfano huu.