Hazel Crane
Hazel crane | |
Amezaliwa | 10 November Afrika kusini |
---|---|
Nchi | Afrika Kusini |
Kazi yake | Mfanyabiashara namtunzaji kumbukumbu za watu walio fariki |
Hazel Crane (1951 – 10 Novemba 2003) alikuwa mashuhuri katika itikadi ya Ujamaa, mfanyabiashara na mtunzaji kumbukumbu za watu waliofariki kutokea Afrika Kusini. Aliuawa karibu na jumba lake la kifahari kaskazini mwa jiji la Johannesburg mtaa wa Abbotsford, mtaa huohuo ambamo aliyekuwa tajiri wa madini Brett Kebble aliuawa mnamo mwaka 2005.[1]
Maisha ya Awali
[hariri | hariri chanzo]Akizaliwa kama Hazel Elizabeth Magee huko Belfast, Ireland Kaskazini, alihamia Rhodesia[2] akiwa mtoto na baadaye Afrika Kusini akiwa mtu mzima. Akiwa Afrika Kusini alijihusisha na kamati mbalimbali za kihisani na miradi, kama vile ufadhili wa elimu kwa watoto maskini.[3]
Maisha ya Baadaye
[hariri | hariri chanzo]Hapo awali, Crane aliolewa na Anthony Crane, ambaye aliuawa akiwa na umri wa miaka 25 wakati wa vita za msituni za Rhodesia. Wawili hao tayari walikuwa na mtoto mmoja, na wakati wa kifo cha mumewe, Crane alikuwa ana mimba ya mtoto wa pili.[2] Baadaye alikua na ndoa yenye misukosuko na bwana Shai Avissar aliyekua na tuhuma za kuongoza kikundi cha kimafia cha Israeli. Wakati kifo kinampata bwana Shai mnamo mwaka 1999, wawili hao walikua wameshatengana.[2]
Alikua rafiki wa karibu wa Winnie Mandela, ambaye alihudhuria msiba wake na ndiye aliyekua mpambe wake wakati wa harusi yake na bwana Avissar. Crane alifuatana na Winnie Mandela wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake kabla ya kamati ya ukweli na makubaliano kuundwa.[3]
Kifo na Urithi
[hariri | hariri chanzo]Crane alipigwa risasi akiwa katika gari lake mnamo Novemba mwaka 1999, akiwa anaelekea mahakamani kusikiliza kesi dhidi ya Saat aliyetuhumiwa kumuua mume aliyepita wa bi Crane karibu na Sunninghill mwishoni mwa mwaka 1999.[4] Crane aliambatana na mwanamke ambaye alipigwa risasi mkononi, uchunguzi wa polisi ulibani kuwa shambulio hilo lilimlenga Crane moja kwa moja, ambaye alipigwa risasi ya kichwa, mguu, kifua na mkono [5] Baadye taarifa zilitoka ya kwamba bi Crane alitarajiwa kutoa ushuhuda dhidi ya Saat na chanzo cha karibu na Crane kilisema alijua mengi sana, angeweza kutambua na kutaja wengi waliohusika katia mauaji ya bwana Saat.[6] Alikuwa ndiye shahidi wa tatu katika kesi ya mauaji ya bwana Saat, ambaye ilisemekana aliuwawa na John van Loggerenberg maarufu kama "Johnna" ambaye inasadikika alikuwa mwanachama wa kikundi cha kimafia cha Sicilian, madai ambayo hakuwahi kukataa wala kukubali. Polisi walidai kwamba alihusika pia katika mauaji ya Giulio Bascelli na Carlo Binne.; Giulio Bascelli alipigwa risai kichwani katika karakana iliyotelekezwa muda mfupi baada ya kifo cha Avassi mnamo mwaka 2000, Carlo Binne alipigwa risasi na kufa papo hapo akiwa Gecko Lounge, klabu ya usiku huko Johannesburg mnamo Aprili mwaka 2008.[7]Kikundi cha Kimafia cha Sicillian, kilikuwa nyuma ya mauaji ya watu mashuhuri ikijumuisha mawakili, mashahidi na majaji. van Loggerenberg hakuwahi kuhukumiwa kwa mauaji yoyote kutokana na ukosefu wa Ushahidi unaomuunganisha na mauaji hayo.
Kabla ya kifo chake, Crane alikuwa akifanya kazi na muandishi wa kiingereza, David Kray juu ya kumbukumbu zake. Bayografia ya, Hazel Crane: Testimony from Beyond the Grave[3] ilichapishwa mwaka 2004 na ilijumuisha mambo mengi ya kushangaza kuhusu safari yake iliyopita. Kitabu hicho kinaelezea Maisha binafsi ya kihalifu ya Crane. Alipata utajiri wake kwa kuuza Almasi na Zumaridi kimagendo, akifanya soko haramu, akimiliki kituo cha picha za uchi na video za ngono. Alielezea pia ni kwa jinsi gani aliwahi kuingia katika chimbo la chini ya ardhi na kukutana na "Johnna" kujadili juu ya usalama wake na njia zake za usafirishaji. [2] Kabla ya Maisha ya uhalifu, alijifunza uhudumu wa afya na baadaye akawa mfanyabiashara. Wakati akifanya biashara ya uuzaji haramu wa almasi, aliunda kikundi chenye nguvu akiwa na washiriki kutoka Johannesburg ambao walimlipa kwa, fedha za kigeni ambazo alizitumia kuanzisha biashra mbalimbali mojawapo ni mgahawa wenye mafanikio wa Copa Cobana, Sehemu mashuhuri sana nchini Rhodesia.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Gill Gifford, "Kebble and Hazel Crane murdered in same area", IOL (South Africa), 28 September 2005.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 "High society rocked by the shady past of one of its own". The Age. 24 Desemba 2004.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 Kray, David; Crane, Hazel (2004). Hazel Crane: Testimony from Beyond the Grave. New Africa Books.
- ↑ "Socialite dies after shooting". News24. 10 Novemba 2003. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-21. Iliwekwa mnamo 2021-04-17.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Hazel Crane killed in attack". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Februari 2009. Iliwekwa mnamo 21 Septemba 2008.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ ""Hazel knew too much"". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Februari 2009. Iliwekwa mnamo 21 Septemba 2008.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kutokana na kukosekana kwa Ushahidi, mahakama kuu ilifutilia mbali kesi zote dhidi ya van Loggerenberg. Inaaminika kwamba van Logerenberg alipanga na kutekeleza mauaji ya watu wengi wenye majina makubwa. Orodha ya waliouwawa inajumuisha mawakili, wakusanya madeni na wauza madawa ya kulevya kutoka sehemu mbalimbali za nchi za Ulaya na Afrika, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na bwana Paul O’Sullivan. "Israeli gangsters blamed for murder of Winnie's friend"
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hazel Crane kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |