Mkoa wa Haut-Ogooué
Haut-Ogooué ni moja kati ya mikoa tisa nchini Gabon. Mkoa umepewa jina baada ya Mto Ogooué. Mkoa umechukua eneo la kilomita za mraba zipatazo 36,547. Mji mkuu wa mkoa huu ni Franceville. Miongoni mwa viwanda vyake vikubwa ni pamoja na machimbo ya madini, pamoja na manganisi, dhahabu na urani nazo zinapatikana kwenye mkoa huu. Hapa ni nyumbani pa kihistoria kwa tamaduni tatu, kina Obamba, Ndzabi na Téké. Kama jinsi ilivyo mikoa mingi katika Afrika, matumizi mengi ya jadi katika ardhi yametupiliwa mbali na kukaribisha ujenzi wa miji mikubwa vijijini.[1] Mnamo mwezi wa Agosti 2006, klabu yake soka imeshinda Kombe la Uhuru la Gabon.[2]
Kwa upande wa kaskazini-mashariki, mashariki, na kusini, Haut-Ogooué imepakana na mikoa kadhaa ya Jamhuri ya Kongo:
- Cuvette-Ouest - kaskazini-mashariki
- Cuvette - mashariki
- Plateaux - kusini-mashariki
- Lékoumou - kusini
- Niari - kusini-magharibi
Kwa nyumbani, mkoa umepakana na mikoa ifuatayo:
- Ogooué-Lolo - magharibi
- Ogooué-Ivindo - kaskazini
Departments
[hariri | hariri chanzo]Haut-Ogooué imegawanyika katika departments 8:
- Djoue Department (Onga)
- Djououri-Aguilli Department (Bongoville)
- Lekoni-Lekori Department (Akieni)
- Lekoko Department (Bakoumba)
- Lemboumbi-Leyou Department (Moanda)
- Mpassa Department (Franceville)
- Plateaux Department (Leconi)
- Sebe-Brikolo Department (Okondja)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "matumizi mengi ya jadi katika ardhi yametupiliwa mbali na kukaribisha ujenzi wa miji mikubwa vijijini". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-03-03. Iliwekwa mnamo 2010-10-08.
- ↑ "Pan Express Yanyakua Kombe la Uhuru la Gabon". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-03-11. Iliwekwa mnamo 2021-10-24.
1°38′S 13°35′E / 1.633°S 13.583°E
Makala hii kuhusu maeneo ya Gabon bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkoa wa Haut-Ogooué kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |