Hakim Ziyech

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hakim Ziyech (2020)

Hakim Ziyech (kwa Kiarabu: حكيم زياش; alizaliwa 19 Machi 1993) ni mchezaji wa soka wa Moroko ambaye anacheza kama kiungo mshambuliaji wa Chelsea F.C. ya Uingereza na timu ya taifa ya Moroko.

Mnamo 2019, alichaguliwa kama mmoja wa wachezaji bora 20 katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya (UEFA) kwa msimu wa 2018-19. Anajulikana kwa kufunga kwake, kukimbiza mpira, kupiga pasi ndefu, na kupiga faulo nzuri.

Ziyech alianza kazi yake ya kitaaluma katika klabu ya Uholanzi Heerenveen mwaka 2012. Msimu wa 2015-16 ulikuwa mkubwa sana kwa Ziyech, kwa kuwa alifunga mabao 17 na kutoa msaada 10 katika ligi ile. Mnamo mwaka 2016, Ziyech alijiunga na Ajax kwa mkataba wa miaka mitano kwa ada ya milioni 11.

Ziyech alistahili kuchezea timu ya taifa ya Uholanzi au Moroko. Mwaka 2015, alithibitisha kuwa ataiwakilisha Morocco katika ngazi ya kimataifa. Alichaguliwa katika kikosi cha wanaume 23 katika Kombe la Dunia la 2018, pia ameiwakilisha nchi yake katika Afcon 2019.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hakim Ziyech kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.