Hadja Idrissa Bah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hadja Idrissa Bah
Hadja Idrissa Bah
Hadja Idrissa Bah
Alizaliwa 23 Agosti 1999
Kazi yake mwanaharakati

Hadja Idrissa Bah (pia: Hadja Idy; alizaliwa 23 Agosti 1999) ni mwanaharakati wa kike wa haki za watoto kutoka Guinea, ambaye alichaguliwa kuwa rais wa bunge la watoto wa Guinea mwaka 2016. Pia alikuwa mshauri wa Rais Emmanuel Macron kwenye masuala ya wanawake.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Wazazi wake walifanya kazi ya kuuza duka na kufanya usafi, walimsaidia kutimiza ndoto zake za kuhitimu masomo ya sekondari katika shule ya Saint Georges High School huko Conakry.[1] Alisomea sayansi ya siasa kwa mwaka mmoja katika chuo cha University of General Lansana Conté (fr:Université Général Lansana Conté|fr), kabla ya kudahiliwa kwenye kitivo cha sheria katika chuo Sorbonne University (Paris).

Uanaharakati[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2016 Bah alichaguliwa kuwa Rais wa bunge la watoto wa Guinea. Kama Rais, aliwataka viongozi wa Guinea kuheshimu haki za watoto: "Haki za mtoto wa Guinea zipo hatika hali ya kutisha, kwa sababu wanasahauliwa."[2] Anajihusisha haswa na vita dhidi ya ukeketaji wa wanawake, cha kukatisha tamaa juu jambo hili ni kwamba "imani potofu zina uzito zaidi ya sheria".[3] Katika kipindi chake cha urais aliongelea waziwazi mambo mbalimbali, ikiwemo: kupinga ndoa za utotoni (teen marriage);[4] sexual and (domestic violence);[3] ubakaji;[5] unyanyapaa wa kijinsia dhidi ya wanawake.[6] Bah alichaguliwa kwenye bunge akiwa na miaka 13.[7]

Mwaka 2016 alianzisha (Guinea Girl Leaders Club), ambayo ilitambua manyanyaso wanayokutana nayo mabinti na wasichana wadogo katika jamii ya watu wa Guinea.[3] Taasisi ilijikita kuwaelimisha wasichana wadogo ambao wanarubuniwa kufunga ndoa katika umri mdogo ili kufikiria mara mbili kabla ya kukubali.[8] Kundi lake lilipingana na wazazi wanaowashawishi mabinti zao kuolewa katika umri mdogo.[9] Pia walianzisha kampeni dhidi ya ukeketaji female genital mutilation, kwa kuzingatia zaidi nyakati za likizo za shule kwenye msimu wa joto - muda ambao mabinti wengi wanakeketwa.[10]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Le respect du droit des enfants :un combat de Idrissa Bah présidente du parlement des enfants de Guinée". archive.wikiwix.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-03-05. Iliwekwa mnamo 2021-03-05.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
  2. "VIDEO: portrait of Hadja Idrissa Bah, a young Guinean who fights against underage marriage". archive.wikiwix.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-02-07. Iliwekwa mnamo 2021-03-05.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
  3. 3.0 3.1 3.2 "HADJA IDRISSA BAH, SON COMBAT POUR LES DROITS DES JEUNES GUINÉENNES !". archive.wikiwix.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-09. Iliwekwa mnamo 2021-03-05.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
  4. "Des ados contre le mariage précoce". BBC News Afrique (kwa Kifaransa). 2018-10-24. Iliwekwa mnamo 2021-03-05. 
  5. Anonym. "Hadja Idrissa Bah, anti-excision activist and "breaker of early marriages" | tellerreport.com". www.tellerreport.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-03-05. 
  6. Chabo, Elena (2019-11-26). "Inspiring young activists speaking up around the world". Stylist (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-03-05. 
  7. "Hadja Idrissa Bah, une jeunesse contre les violences faites aux femmes", Le Monde.fr, 2018-12-30. (fr) 
  8. Peyton, Nellie. "Teenage girls step in to stop child marriages in West Africa", Reuters, 2017-10-27. (en) 
  9. "These Teen Girls Are Stopping Child Marriages in West Africa". Global Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-03-05. 
  10. "Young Guinean activists want to end FGM during summer break". The Observers - France 24 (kwa Kiingereza). 2019-07-04. Iliwekwa mnamo 2021-03-05. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hadja Idrissa Bah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.