Nenda kwa yaliyomo

Emmanuel Macron

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Emmanuel Macron
Emmanuel Macron in 2017

Rais wa Ufaransa (2017)
hadi 2016 Waziri wa Uchumi
Muda wa Utawala
26 August 2014 – 30 August 2016
Waziri Mkuu Manuel Valls
mtangulizi Arnaud Montebourg
aliyemfuata Michel Sapin

tarehe ya kuzaliwa 21 Desemba 1977 (1977-12-21) (umri 47)
Amiens, Ufaransa
chama En Marche! (2016–present)
chamakingine Chama cha Kisoshalisti cha Ufaransa (2006–2009)
ndoa Brigitte Trogneux (m. 2007–present) «start: (2007)»"Marriage: Brigitte Trogneux to Emmanuel Macron" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Emmanuel_Macron)
mhitimu wa Paris X Nanterre
Sciences Po
École nationale d'administration

Emmanuel Jean-Michel Frédéric Macron (alizaliwa Amiens, 21 Disemba 1977) ni mwanasiasa nchini Ufaransa ambaye mwaka 2017 alichaguliwa na wananchi kuwa rais wa taifa. Akiwa na umri wa miaka 39, Macron akawa rais mdogo zaidi katika historia ya Ufaransa

Familia na maisha ya binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Macron alizaliwa katika familia ya madaktari akapata elimu yake katika shule ya kikatoliki na baadaye katika vyuo vikuu hadi shahada ya uzamili akaendelea katika chuo cha utawala wa kitaifa na kujiunga na utumishi wa serikali katika wizara ya fedha.

Alipokuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari alianzisha uhusiano wa karibu na mwalimu wake wa kike Brigitte Trogneux aliyemzidi kiumri miaka 24[1]; wazazi wake ambao hawakukubali uhusiano huu walimtuma kijana kusoma shule nyingine mjini Paris lakini kijana na mwalimu waliendelea na uhusiano na hatimaye walifunga ndoa mwaka 2007[2]. Hawakuzaa watoto wa pamoja lakini Brigitte ana watoto watatu kutoka kwa ndoa yake ya awali na wawili ni wakubwa kumshinda mumewe.

Maisha ya kisiasa

[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa kufanya kazi serikalini alikuwa mwanachama wa Chama cha Kisoshalisti cha Ufaransa (Parti Socialiste – PS) kuanzia 2006 hadi 2009. Mwaka 2008 alitoka katika utumishi wa serikali na kujiunga na benki ya Rothschild. Mwaka 2012 alihamia katika ofisi ya rais wa Ufaransa Francois Hollande akiwa naibu katibu mkuu wa ofisi hii. 2014 aliendelea kuwa waziri wa uchumi, viwanda na teknolojia wa Ufaransa.

Mwaka 2016 Macron aliunda chama kipya cha La République En Marche na baada ya kukusolewa kwa hatua hii na rais Hollande alijiuzulu katika serikali akatangaza kuwa atagombea urais katika uchaguzi wa 2017[3] [4].

Katika kampeni ya uchaguzi Macron alishika muda mrefu nafasi ya tatu lakini baada ya kashfa za mgombea mwenzake François Fillon kutoka mkondo wa de Gaulle alisogea mbele. Alishinda katika awamu la kwanza la uchaguzi pamoja na Marie Le Pen mgombea wa chama cha Front National. Katika kura ya awamu la pili alishinda kwa asilimia 66 za kura za wananchi.[5]