Gamalieli
Mandhari
Gamalieli alikuwa kiongozi wa kabila la Manase anayetajwa katika Biblia ya Kiebrania, ambayo ni sehemu ya Biblia ya Kikristo (Agano la Kale), katika kitabu cha Hesabu, sura ya 2, mstari wa 20.
Muhimu zaidi ni Gamalieli mwingine, Gamalieli I au Gamalieli mzee, kiongozi wa Mafarisayo katika karne ya 1 B.K. Anatajwa katika Agano Jipya, ambayo ni sehemu ya pili ya Biblia ya Kikristo, kama mwalimu wa mtume Paulo aliyewatetea mitume wa Yesu. Katika Mdo 5:34-39 anaonekana kama msemaji wa Mafarisayo na Mwalimu wa Torati anayepinga jitihada za Masadukayo kuua Petro na mitume wengine.
Kutokana na taarifa hiyo mapokeo ya Ukristo yanamheshimu kama mtakatifu. Katika Talmud ya Uyahudi anatajwa kwa heshima kama Rabban Gamliel.
Tazama pia
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gamalieli kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |