Masadukayo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Masadukayo (kwa Kiebrania צדוקים sadukim) waliunda madhehebu muhimu ya dini ya Uyahudi wakati wa Yesu Kristo. Walikuwa na nguvu hasa kati ya makuhani. Ndiyo maana waliishiwa nguvu hekalu la Yerusalemu lilipoangamizwa na Warumi pamoja na mji mzima mwaka 70 B.K..

Walikubali Torati ya Musa tu, na kukataa vitabu vingine vyote vya Biblia. Kwa msingi huo, walikataa mafundisho yaliyoletwa na manabii, kama vile juu ya ufufuo wa wafu na uzima wa milele[1]. Katika hilo waligongana na Mafarisayo na Yesu ambaye, kadiri ya Injili, ndio waliohusika zaidi na kifo chake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]