Gabriel Jesus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gabriel Jesus

Gabriel Fernando Jesus (alizaliwa 3 Aprili 1997[1][2]) ni mchezaji wa soka wa Brazil ambaye anacheza katika klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Arsenal na timu ya taifa ya Brazil. Gabriel anacheza kama mshambuliaji katika ngazi ya klabu na katika timu ya taifa.

Jesus alianza kazi yake huko Palmeiras. Alipigwa kura kuwa mgeni bora wa 2015 katika michuano ya Brazil na Serie A, mwaka ambao pia alisaidia timu yake kushinda Copa do Brasil.

Mwaka uliofuata aliitwa kuwa mchezaji wa msimu huko Palmeiras, alishinda cheo cha kwanza cha ligi ya kitaifa akiwa na miaka 22[3][4]. Alijiunga na Manchester City mwezi Januari 2017 kwa ada ya milioni 32, na alishinda Ligi Kuu na EFL Cup mwaka 2018.[5]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Gabriel Jesus: Overview. ESPN.
  2. Gabriel Jesus: Profile. HEIM:SPIEL.
  3. PTD fala com Gabriel Fernando, destaque do sub-17 (pt). Palmeiras Todo Dia (4 August 2014).
  4. Famoso na base, Gabriel Jesus é "fenômeno" do Palmeiras (pt). Globo Esporte (1 January 2015).
  5. Gabriel Jesus (en). www.arsenal.com. Iliwekwa mnamo 2023-02-26.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gabriel Jesus kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.