Nenda kwa yaliyomo

Florensiani wa Midila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Florensiani wa Midila (alifariki baada ya 484) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki katika mji wa Midila (leo Mdila nchini Algeria).

Aliteswa akapelekwa uhamishoni kwenye kisiwa cha Corsica (leo nchini Ufaransa) katika dhuluma ya Huneriki, mfalme wa Wavandali[1].

Habari zake zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Novemba[2][3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.