Nenda kwa yaliyomo

Huneriki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sarafu ya Huneriki.

Huneriki (alifariki 23 Desemba 484) alikuwa mtoto wa kwanza wa Genseriki, mfalme wa Wavandali na Waalani kwa karibu miaka 50 (428477) ambaye aliinua makabila haya madogo kuwa ufalme imara katika Afrika Kaskazini uliotikisa Dola la Roma Magharibi katika karne ya 5 hata kuteka jiji hilo kwa muda mnamo Juni 455.

Huneriki hakuendeleza mipango mikubwa ya baba yake lakini, baada ya muda[1][2], alizidi kudhulumu kikatili Wakatoliki wa Afrika Kaskazini[3] hivi kwamba Waarabu Waislamu walipoiteka Ukristo ulikoma haraka.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Malchus, fragment 13. Translated by C.D. Gordon, Age of Attila: Fifth Century Byzantium and the Barbarians (Ann Arbor: University of Michigan, 1966), p. 125f
  2. Victor of Vita, 2.3-6; translated by John Moorhead, Victor of Vita: History of the Vandal Persecution (Liverpool: University Press, 1992), pp. 25f
  3. "Saint Patrick's Church: Saints of March 23". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-06-13. Iliwekwa mnamo 2020-11-09.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Huneriki kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.