Filipo II wa Masedonia
Filipo II wa Masedonia[1] (kwa Kigiriki: Φίλιππος Β΄ ὁ Μακεδών, Phílippos II ho Makedṓn; 382 KK – 336 KK) alikuwa mfalme wa Masedonia katika Ugiriki wa Kale kuanzia mwaka 359 KK hadi alipouawa.
Mnamo 500 KK kulikuwako ufalme ulioitwa Masedonia ambao ulihesabiwa kama sehemu ya utamaduni wa Ugiriki wa kale na wafalme waliruhusiwa kwenye michezo ya Olimpiki ya madola ya Wagiriki.
Pamoja na sehemu nyingi za Ugiriki ufalme huo ulipaswa kukubali ubwana wa Milki ya Uajemi, lakini Filipo alifaulu kuurudisha uhuru akaendelea kuifanya Masedonia kuwa dola kiongozi kati ya madola madogo ya Ugiriki.
Mwanawe Aleksanda Mkuu aliimarisha utawala wake juu ya Wagiriki wengine na kushambulia Milki ya Uajemi na hatimaye kuivamia na kuishinda kwa jeshi kutoka sehemu zote za Ugiriki.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Philip II of Macedonia: Ian Worthington, Yale University Press, ISBN 0300164769, 9780300164763
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- A family tree focusing on his ancestors
- A family tree focusing on his descendants Ilihifadhiwa 6 Oktoba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Plutarch: Life of Alexander
- Pothos.org, Death of Philip: Murder or Assassination?
- Philip II of Macedon entry in historical source book by Mahlon H. Smith
- Twilight of the Polis and the rise of Macedon (Philip, Demosthenes and the Fall of the Polis). Yale University courses, Lecture 24. (Introduction to Ancient Greek History)
- The Burial of the Dead (at Vergina) or The Unending Controversy on the Identity of the Occupants of Tomb II
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Filipo II wa Masedonia kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |