Filipo GaoLubua
Filipo GaoLubua (pia anajulikana kwa jina la Filipo Lubua; alizaliwa Mkoa wa Kilimanjaro, na kukulia mjini Arusha, Tanzania) ni mwandishi wa riwaya na mshairi kutoka Tanzania.
Aliandika riwaya iitwayo Kilele Kiitwacho Uhuru pamoja na diwani kadha wa kadha za ushairi.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kuhitimu elimu ya juu ya sekondari mwaka 2006, alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutunukiwa shahada ya kwanza katika Sanaa na Elimu (B.A.Ed.) mwaka 2009, ambako alitaalamikia masomo ya Jiografia na Isimu.
Mwaka 2010, alikwenda Chuo Kikuu cha Wisconsin Madison, Marekani, kama mwalimu wa Kiswahili kupitia ufadhili wa nchi ya Marekani chini ya programu maarufu ya Fulbright.
Baada ya programu hiyo, mwaka 2012 alijiunga na Chuo Kikuu cha Ohio, kwa masomo ya umahiri katika Isimu Tumizi, akitaalamikia Ufundishaji na Ujifunzaji wa Lugha kwa Kompyuta (UULUKO).
Baada ya masomo ya umahiri mwaka 2014, alijiunga na programu ya uzamivu na mwaka 2019 alitunukiwa digrii ya uzamivu (Ph.D.) katika masuala ya Teknolojia ya Elimu (Instructional Technology).
Kwa sasa ni profesa katika Idaya ya Isimu ya Chuo Kikuu cha Pittsburgh na Rais wa Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) Archived 18 Aprili 2024 at the Wayback Machine..
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Filipo GaoLubua kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |