Eutikyo shemasi mdogo
Mandhari
(Elekezwa kutoka Eutikyo)
Eutikyo (alifariki 356) alikuwa shemasi mdogo wa Aleksandria (Misri) aliyeteswa wakati wa Kwaresima kwa sababu ya kushika imani sahihi dhidi ya Uario. Hivyo, walipompeleka kufanya kazi migodini, alifariki njiani.
Patriarki Athanasius amesimulia mateso yake na ya wengine wengi katika mwaka huo yaliyohimizwa na Joji, askofu mpinzani wake.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Machi[1][2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |