Estrojeni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Estrojeni (kutoka neno la Kiingereza "estrogen" lenye asili ya Kigiriki: οἶστρος, oistros, linaloweza kudokeza "hamu ya ngono" na kiambishi tamati γεν, gen, "sababishi") ni homoni ya kike muhimu zaidi ambayo imo mwenye mwili wa wanyama aina ya Chordata (wenye uti wa mgongo) na baadhi ya wadudu. Jina estrojeni pia linaweza kutumika kwa kitu chochote ambacho chaiga homoni hii ya estrojeni kama vile dawa ambazo hupewa wanawake ili wawe na ashiki ya ngono.

Katika binadamu, homoni hii ni muhimu hasa kwa wanawake na hutunzwa kwenye ovari, ini na huwasaidia wanawake wajawazito, huwasaidia wasichana kwenye ukuaji, husaidia pia kwenye kipindi cha ovulasheni. Wakati wa hedhi kwisha kabisa kiwango cha estrogeni hushuka.

Kazi ya estrojeni[hariri | hariri chanzo]

Kukua kwa matiti ya wasichana haswa wakiwa katika umri wa kubalehe. Homoni ya estrojeni zikishirikiana na homoni ya ukuzi (human growth hormone) husaidia katika ubalehe wa wasichana ambapo matiti yao madogo yaanza kunenepa na kuwa makubwa. Estrojeni pia husaidia kufanya mafuta yagawanyike sawa katika msichana anayebalehe ili awe wa kuvutia na mwenye ngozi nyororo. Homoni hii pia huwafanya wasichana waanze kupata matako yaliyowanda.

Estrojeni hufanya uke wa msichana uwe umekomaa ili awe tayari kushiriki katika ngono na pia kushika mimba. Homoni hii huwafanya wasichana wapate uchu wa ngono, au ashiki ya mapenzi na kwa njia hii huonekana kama homoni ya uzazi wa wanawake.

Estrojeni pia husaidia mama anapokuwa mjamzito ili matiti yake yawe tayari kutoa maziwa ya kunyonyesha mtoto

Usawa wa estrojeni na tesistosteroni[hariri | hariri chanzo]

Kinyume cha homoni ya estrojeni ni homoni ya tesistosteroni ambayo inapatikana san asana kwa wanaume. Hata hivyo, wanawake wako na kiwango fulani cha tesistosteroni ilhali wanaume nao wana kiwango fulani cha estrojeni. Tofauti ni kwamba wanawake wana estrojeni nyingi zaidi mwilini ikilinganishwa na tesistosteroni ilhali wanaume nao wana kiwango kikubwa cha tesistosteroni ikilinganishwa na estojeni.

Mtoto mchanga anapozaliwa, awe wa kiume au kike, huwa na estrojeni nyingi sana mwilini na ndio maana huwa na jinekomastia. Hii hufanyika maana homoni ya estrojeni hutoka kwa mama mzazi hadi kwa mtoto. Jinekomastia hii huisha mtoto anapozaliwa na kukaa kwa muda fulani.

Jinekomastia pia hupatikana kwa wanaume walio na umri wa miaka thelathini kwenda juu wanpokuwa na estrojeni nyingi mwilini. Ili kumaliza matiti haya, wao hushauriwa wanywe dawa za kuongeza tesistosteroni mwilini kama crazy bulk, marine muscle na testogen au wafanywe operesheni ya liposuction au mastectomy ili ufuta uliokuwa kwa matiti haya utolewe.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

  1. Crazy bulk
  2. Marine muscle
  3. Testogen
  4. http://studentorganisations.uonbi.ac.ke/ccpe/
  5. http://mwalii.co.ke
Morpho didius Male Dos MHNT.jpg Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Estrojeni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.