Nenda kwa yaliyomo

Kibwirosagi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Eminia)
Kibwirosagi
Kibwirosagi kichwa-cheusi
Kibwirosagi kichwa-cheusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Cisticolidae (Ndege walio na mnasaba na videnenda)
Sundevall, 1872
Ngazi za chini

Jenasi 7 na spishi 9 za vibwirosagi:

Vibwirosagi ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Cisticolidae. Wanafanana na videnenda lakini mkia wao ni mrefu zaidi na wana rangi kali zaidi: nyekundu, kijani, kahawia na/au kijivu mgongoni na njano, nyekundu, marungi, hudhurungi na/au kijivu chini. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara katika misitu na mapori. Hula wadudu. Hulijenga tago lenye kuba ya manyasi, majani na/au vigoga katika kichaka, mmea au dege la watoto. Jike huyataga mayai 1-4.