Emau
Emau ni kijiji kilichotajwa katika Injili ya Luka katika Agano Jipya. Mwinjili Luka anaandika kuwa Yesu alionekana huko baada ya mauti na ufufuko wake mbele ya Kleofa na mwenzake walipokuwa wakitembea katika njia iliyoelekea Emau.
Utambulisho wake wa kijiografia si wazi, maeneo kadhaa yamependekezwa katika historia. Inajulikana tu kwamba ilikuwa imeunganishwa na barabara ya kwenda Yerusalemu; umbali uliotolewa na Mwinjili Luka unatofautiana katika hati tofauti na takwimu iliyotolewa imefanywa kuonekana ngumu zaidi na watafsiri.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Jina la mahali Emau ni la kawaida katika vyanzo vya zamani vya Mashariki ya Kati na kawaida hutoholewa kataka lugha ya Kigiriki na ya Kilatini kutoka neno la Kisemiti la "chemchemi ya joto", kwa Kiebrania ni hamma au hammat (חמת). Huko zamani na leo, chemchemi nyingi zinaitwa Hama, Hamath na tofauti zake. [1]
Kwa sasa inadhaniwa kujulikana kama ni Motza.
Emau katika Agano Jipya
[hariri | hariri chanzo]Luka 24:13-35 inahubiri kwamba Yesu anaonekana baada ya kufufuka kwake kwa wanafunzi wawili ambao wanatembea kutoka Yerusalemu kwenda Emau, ambayo inaelezewa kuwa ni stadiia 60 (km 10.4 hadi 12 kulingana na ufafanuzi gani wa stadion unatumika) kutoka Yerusalemu. Mmoja wa wanafunzi anaitwa Kleopa (aya ya 18), wakati mwenzake hatajwi jina.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Emau kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |