Elmina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ngome ya Elmina.

Elmina ni mji wa Jamhuri ya Ghana, Mkoa wa Kati. Elmina iko kwenye mwambao wa Ghuba ya Guinea ambayo ni pwani ya kusini ya Ghana, takriban kilomita 12 upande wa magharibi wa Cape Coast.

Katika sensa ya mwaka 2013 kulikuwa na wakazi 33,576[1]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Elmina ilifikiwa na Wareno mara ya kwanza mnamo mwaka 1471 walipokuta biashara ya dhahabu iliyoendeshwa baina ya wenyeji na wafanyabiashara Waarabu. Hivyo wakaita mji "mina" yaani mgodi kwa sababu walichukua hapa dhahabu. Wareno walijenga kituo wakaendelea kushiriki katika biashara hiyo na mwaka 1481 walijenga Ngome ya Elmina (Castelo de São Jorge da Mina). Ngome hiyo ilikuwa makao makuu ya Wareno kwenye pwani ya Afrika Magharibi hadi kutwaliwa na Waholanzi mnamo 1637 walioendelea kuitumia hadi mwaka 1872 walipoiuza kwa Waingereza.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. World Gazetteer online. World-gazetteer.com.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Elmina kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.