Ngome ya Elmina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ngome ya Mt. George.
Ngome ya Elmina kadiri ya Blaeu-Van der Hem Atlas (miaka ya 1660).

Ngome ya Elmina ilianza kujengwa na Wareno mnamo mwaka 1482 ikifahamika kama Castelo de São Jorge da Mina (Kasri ya madini ya mtakatifu George), pia kwa jina la Castelo da Mina au Mina (Feitoria da Mina), na hivi sasa inafahamika kwa jina la Elmina, Ghana (zamani Pwani ya Dhahabu).

Lilikuwa kituo cha kwanza cha kibiashara kuanzishwa huko Ghuba ya Guinea, na ni jengo la zamani sana lenye muundo wa Ulaya kuwepo kusini kwa Sahara.[1] Awali iliimarishwa kama makazi ya biashara, kisha baadae kasri hiyo ikawa moja kati ya kituo cha muhimu kwenye msafara biashara ya utumwa ya Atlantic .Dutch walichukua jumba hilo kutoka kwa wareno mnamo mwaka 1637, baada ya najaribio ya kwanza yaliyogonga mwamba mwaka 1596, pia wakapata umiliki wa Pwani yote ya dhahabu and took over all of the pwani ya dhahabu ya wareno mwaka 1642. Biashara ya utumwa iliendelezwa na wadachi mpaka mwaka 1814. Kisha mwaka 1872,pwani ya dhahabu y wadachi, ikiwemo na majumba, zikawa miliki za waingereza kutawala.[2]

Pwani ya dhahabu, ambao kwa sasa inafahamika kama Ghana, ikapata uhuru mnamo mwaka 1957 kutoka kwa waingereza, ndipo ikapata uwezo wakusimamia kasri.[3] Kasri ya Elmina ni eneo la kihistoria na ni eneo muhimu lililotumika na msanii Werner Herzog mnamo mwaka 1987 kufanyia kazi zake za filamu Cobra Verde. Kasri hii inatambulika na chama cha UNESCO kama Urithi wa dunia.[4] Pia ni kivutio cha watalii mjini Ghana.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]