Nenda kwa yaliyomo

Eli Wallach

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eli Wallach, mnamo 1966.

Eli Herschel Wallach (7 Desemba 1915 – 24 Juni, 2014) alikuwa mwigizaji wa filamu, televisheni, na jukwaani kutoka Jiji la New York nchini Marekani. Alitambulika kwa nafasi zake kama mwigizaji mwenye vitabia fulani tata hivi. Kazi yake ya burudani ilidumu kwa zaidi ya miongo sita. Amewahi kupata Tuzo ya BAFTA, Tuzo ya Tony, na Tuzo ya Emmy ya Primetime. Pia alijumuishwa katika American Theater Hall of Fame mnamo 1988 na kupokea Tuzo ya Heshima ya Academy mnamo 2010.[1][2]

Akiwa amefunzwa awali katika maigizo ya jukwaa, alipata zaidi ya nyusika 90 katika filamu. Yeye na mke wake Anne Jackson mara nyingi walionekana pamoja katika jukwaa, hatimaye wakawa wanandoa maarufu wa uigizaji katika maigizo ya Marekani. Awali Wallach alisomea sanaa ya maigizo chini ya Sanford Meisner na baadaye akawa mshirika mwanzilishi wa Actors Studio, ambapo alifundishwa na Lee Strasberg. Aliigiza aina mbalimbali za nyusika katika taaluma yake, hasa kama mwigizaji msaidizi. Alishinda Tuzo ya Tony kama mwigizaji bora msaidizi katika igizo la The Rose Tattoo (1951).

Kwa uigizaji wake wa kwanza katika filamu Baby Doll (1956), alishinda Tuzo ya BAFTA na kupata teuzi katika Tuzo za Golden Globe. Miongoni mwa nyusika zake maarufu zaidi ni Calvera katika The Magnificent Seven (1960), Guido katika The Misfits (1961), na Tuco ("The Ugly") katika The Good, the Bad and the Ugly (1966) na Don Altobello katika The Godfather Part III (1990). Filamu zingine mashuhuri ni pamoja na How the West Was Won (1962), Tough Guys (1986), The Two Jakes (1990), The Associate (1996), The Holiday (2006), Wall Street: Money Never Sleeps, na The Ghost Writer (zote mbili 2010).


Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]
Eli akimuweka chini ya ulinzi Clint katika filamu ya The good, the bad and the Ugly.

Filamu Alizocheza

[hariri | hariri chanzo]
  1. http://www.forward.com/articles/eli-wallach-knows-his-lines/ Ilihifadhiwa 16 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.
  2. http://www.filmreference.com/film/80/Eli-Wallach.html

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eli Wallach kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Theater Hall of Fame Adds Nine New Names". The New York Times. Novemba 22, 1988. Iliwekwa mnamo Februari 6, 2019.
  2. "Eli Wallach Appreciation: How Oscar Finally Got It Right After Nearly 60 Years Of No Nominations". Deadline Hollywood. Juni 26, 2014. Iliwekwa mnamo Mei 30, 2023.