Nenda kwa yaliyomo

Nyoka-miviringo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Elapsoidea)
Nyoka-miviringo

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Familia: Elapidae (Nyoka walio na mnasaba na fira)
F. Boie, 1827
Nusufamilia: Elapinae (Nyoka wanaofanana na fira)
Jenasi: Elapsoidea
Ngazi za chini

Spishi 10:

Nyoka-miviringo ni nyoka wenye sumu wa jenasi Elapsoidea katika familia Elapidae. Wamepewa jina hili kwa sababu mwili wao una miviringo mingi, ule wa wachanga hasa.

Nyoka hawa sio warefu sana, sm 80 kwa kipeo. Kichwa ni kifupi na mkia ni mfupi. Wachanga wana miviringo myeupe, kijivu, njano, machungwa au myekundu juu ya rangi msingi ya nyeusi au kahawia. Wakikomaa miviringo inakuwa myeusi zaidi mpaka inapotea kabisa au miviringo myembamba inabaki. Nyoka-miviringo mashariki tu anabakiza miviringo yake.

Nyoka-miviringo hujificha mchana katika vishimo au chini ya majani makavu. Usiku huwinda wakichimba au kuingia vishimo vya wanyama. Hula nyoka wengine, mijusi, nyoka wanafiki, vyura na mayai ya hawa wote.

Sumu ya nyoka-miviringo si kali sana na juu ya hayo hawang'ati kwa kawaida. Kwa hivyo wanaweza kushikwa bila hatari sana. Hata ikiwa mtu anaingizwa na sumu, anapata tu uvimbe wa eneo na kusikia maumivu na kichefuchefu. Dalili hizi zinapotea katika siku 4.

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyoka-miviringo kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.