Nenda kwa yaliyomo

Edward Mrosso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Edward John Mrosso (alizaliwa mkoani Arusha), ni mwanasheria wa Kitanzania na wakili wa kujitegemea ambaye aliwahi kuwa mjumbe wa bodi ya maji mkoa wa Arusha (AUWSA) katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2021. [1] [2]

Mrosso ni mwanasheria na wakili ambaye ni mjumbe wa kamati za kiutawala wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alipata wadhifa huo baada ya kufanyika mchakato wa uteuzi wa chama hicho uliofanyika mnamo mwaka 2019. [3] Katika shughuli za utalii nyanda za juu kaskazini, ni mdau kama mwekezaji na mjasiriamali. [4] Pia ni mwenyekiti wa kamati ya fedha wa Jimbo kuu la kanisa Katoliki Arusha. [5] [6]

Mnamo mwaka 2020, aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii, Hamisi Andrea Kigwangalla alimpongeza Mrosso kwa kuvutia wageni wa nje katika kampeni ya kuhamasisha ongezeko la utalii nchini Tanzania baada ya wimbi la changamoto ya ugonjwa wa uviko-19 (COVID-19) kuathiri uchumi na kupunguza idadi ya watalii wa nje ya nchi. [7] [8]

Mnamo mwaka 2018, Mrosso na mteja wake walikamatwa na vyombo vya sheria kutokana na maagizo ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na baadae kuachiwa huru kwa dhamana. Tukio hili lilihusisha changamoto za kutofuata taratibu na miongozo ya ukiukwaji wa mamlaka za viongozi wa Serikali na wadau wengine katika mimili ya sheria. [9] [10] [11] [12]  [13]

  1. "Board of Arusha Urban Water Supply and Sanitation Authority (AUWSA)" (kwa Kiingereza). The Citizen. 2 Mei 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-06-30. Iliwekwa mnamo 30 Juni 2023. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  2. Junior, Michuzi (5 Mei 2018). "Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jiji la Arusha Aprili 23, 2018 hadi Aprili 22, 2021". Iliwekwa mnamo 30 Juni 2023.
  3. "APPOINTED MEMBERS OF TLS COMMITTEES" (PDF). Tanganyika Law Society.
  4. "Former plantation site turned into a tourist business". Amani Safari Lodges. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-06-30. Iliwekwa mnamo 2023-06-30.
  5. "The Arusha Archdiocesan Finance Committee". Archdiocese of Arusha Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-06-30. Iliwekwa mnamo 2023-06-30.
  6. "NCA annual narrative report on Tanzania" (PDF). Norwegian Church Aid. 30 Mei 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2023-06-30. Iliwekwa mnamo 30 Juni 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Kigwangalla, Hamis [@HKigwangalla] (9 Julai 2019). "Brother Kigwangalla, Congracts ! Your efforts have been noted & appreciated, finally we see results ! Today, we hosted them for lunch. It has been the 1st business after Covid. Edward Mrosso. Amani Restaurant & Lodges. Ahsante sana Ndg. Edward Mrosso,kwa kongole" (Tweet). Iliwekwa mnamo 30 Juni 2023 – kutoka Twitter. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |dead-url= (help)
  8. "Briefing by the Tanzania Minister of Natural Resources Tourism" (PDF) (kwa Kiingereza). Zara Tours. 12 Mei 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2023-05-06. Iliwekwa mnamo 30 Juni 2023. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Ayo, Millard (16 Agosti 2018). "DC Sabaya awasha moto aagiza Mkurugenzi akamatwe kwa ubadhirifu wa Milioni 700". Iliwekwa mnamo 30 Juni 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. Media, Mteza (17 Agosti 2018). "Sabaya ameamuru kukamatwa Mkurugenzi wa TUDELEY na Mwanasheria wake". Iliwekwa mnamo 30 Juni 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Tuhuma za rushwa zamtikisa DC Sabaya", 30 Julai 2019. 
  12. "Wawekezaji wamchongea DC kwa Rais", 12 March 2019. 
  13. "Siasa za Tanzana: Kikwete dhidi ya viongozi wenye tabia za umwamba". BBC Swahili. 11 Oktoba 2019. Iliwekwa mnamo 30 Juni 2023.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Edward Mrosso kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.