Nenda kwa yaliyomo

Edgar F. Codd

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Edgar Frank "Ted" Codd, (19 Agosti, 1923 - 18 Aprili, 2003) alikuwa mwanasayansi wa kompyuta wa nchini Uingereza ambaye, alikuwa akifanya kazi katika shirika la IBM, alivumbua muundo wa uhusiano wa uendeshaji wa hifadhidata, msingi wa kinadharia wa hifadhidata za uhusiano(relational databases) na mifumo ya uendeshaji wa hifadhidata ya uhusiano(relational database management systems). Alitoa michango mingine muhimu katika sayansi ya kompyuta, lakini mtindo wa uhusiano, nadharia ya jumla yenye ushawishi mkubwa wa usimamizi wa data, inabakia kuwa ndio yenye mafanikio yake yaliyotajwa zaidi, kuchambuliwa na kusherehekewa.[1]

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Edgar Frank Codd alizaliwa huko Fortuneswell, Dorset, Uingereza. Baada ya kuhudhuria katika shule ya Poole Gramma, alisomea masuala ya hisabati na kemia katika chuo cha Exeter College, Oxford, kabla ya kufanya kazi kama rubani katika RAF Coastal Command wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Mnamo mwaka 1948, alihamia New York kufanya kazi katika shirika la IBM kama mathematical programmer. Mnamo 1953, akiwa amekasirishwa na Seneta Joseph McCarthy, Codd alihamia Ottawa, Ontario, nchini Kanada. Mnamo 1957 alirejea nchini Marekani na kuendelea kufanya kazi katika shirika la IBM na kuanzia mwaka 1961-1965 alisomea shahada yake ya udaktari katika sayansi ya kompyuta katika Chuo Kikuu cha Michigan huko Ann Arbor.

Miaka miwili baadaye alihamia San Jose, California, kufanya kazi katika San Jose Research Laboratory, ambako aliendelea kufanya kazi hadi miaka ya 1980. [2][3] Aliteuliwa kuwa IBM Fellow katika shirika la IBM mnamo mwaka 1976. Katika miaka ya 1990, afya yake ilizorota na akaacha kufanya kazi.

Codd alipokea tuzo ya Turing (Turing Award) mnamo 1981,[2] na mwaka 1994 alitawazwa kama mmoja wa chama cha Association for Computing Machinery.[4]

Codd alifariki kwa ugonjwa wa moyo nyumbani kwake huko Williams Island, Florida, akiwa na umri wa miaka 79 mnamo 18 Aprili 2003.[5]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Edgar Frank". Author DO Series (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-02-26.
  2. 2.0 2.1 Date, C. J. "A. M. Turing Award – Edgar F. ("Ted") Codd". ACM. Iliwekwa mnamo 2 Septemba 2013. United States – 1981. For his fundamental and continuing contributions to the theory and practice of database management systems.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Rubenstein, Steve. "Edgar F. Codd – computer pioneer in databases." San Francisco Chronicle 24 April 2003: A21. Gale Biography in Context. Web. 1 December 2011.
  4. ACM Fellows https://web.archive.org/web/20090615030959/http://fellows.acm.org/homepage.cfm?alpha=C&srt=alpha |date=15 June 2009 }}
  5. Edgar F Codd Passes Away Archived 4 Juni 2011 at the Wayback Machine., IBM Research, 2003 Apr 23.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Edgar F. Codd kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.