Nenda kwa yaliyomo

Ebedmeleki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ebedmeleki akimuangalia kwa huruma Yeremia ndani ya birika (mchoro wa Jim Padgett, 1984).

Ebedmeleki (kwa Kiebrania: עֶבֶד-מֶלֶךְ, ‘Eḇeḏmeleḵ[1]; kwa Kilatini: Abdemelech) anatajwa katika Kitabu cha Yeremia (sura 38-39) kama afisa Mkushi kwenye ikulu ya mfalme Zedekia wa Yuda wakati wa Yerusalemu kuzingirwa na jeshi la Babuloni (597 KK). Alikuwa towashi[2].

Ebedmeleki alifaulu kumfanya mfalme amruhusu kumtoa nabii Yeremia katika kisima aliposhushwa ili afe humo kwa njaa (38:4–13). Baadaye Yeremia alimuambia kwa niaba ya Mungu kwamba hatauawa katika maangamizi ya Yerusalemu (39:15–18) kwa kuwa alimtumainia.

  1. The name is translated as Servant/Slave of the King, and as such may not be his proper name but a hereditary title.
  2. "www.Bibler.org - Dictionary - Ebed-Melech". Iliwekwa mnamo 2012-12-18.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ebedmeleki kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.