Doreen Peter Noni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Doreen Peter Noni (amezaliwa 10 Machi 1989) ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio Lake FM, jijini Mwanza.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Doreen ni mtoto wa tatu na wa mwisho kuzaliwa na wa kike pekee katika familia ya watoto watatu.[1]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Alisoma shule ya awali ya Upanga. Alihamia Nairobi kuanzia darasa la sita ambapo alisoma mpaka kidato cha sita katika shule ya Brookhouse High School.

Baadae alijiunga na Chuo Kikuu cha Nottingham Trent nchini Uingereza. Huko alisomea mambo ya Multimedia [2]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Ana uzoefu wa zaidi ya miaka mitano katika jukwaa la Multimedia akijihusisha haswa haswa katika uzalishaji wa televisheni na matangazo ya redio.

Lengo lake kubwa ni kutoa mchango katika maendeleo ya jamii na uchumi kwa kutumia mfumo wa radio kibunifu kutatua matatizo ya kijamii yanayoshusha mapato ya raia wanayokutana nayo mara kwa mara.[3] Doreen ana shauku ya kuwezesha vijana na ujasiriamali.

Anajihushisha na programu kadhaa ambazo zinaboresha maisha, anatumia njia bunifu kusaidia kuondoa umaskini na kupaza sauti katika masuala ambayo ni ya kawaida katika jamii kwenye kipindi chake cha redio cha Tena na Tena. Hicho ni kipindi cha elimu na jukwaa la msukumo linalohusisha mahojiano ya vijana ambapo anaongelea masuala ambayo vijana wanakutana nayo na pia kutafuta namna za jinsi ya kutatua matatizo wanayokumbana nayo.

Pindi alipomaliza Mandela Fellowship, alikuwa na mipango ya kutengeneza ngome ya Multimedia Afrika. Anadhamiria kuanzisha kutumia Multimedia kama jukwaa la kusaidia kufungua mzunguko wa umaskini na kusaidia vijana wa Afrika kugundua kusudi lao duniani.[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]