Nenda kwa yaliyomo

Donasyani, Presidi na wenzao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Donasyani, Presidi na wenzao Mansueti, Jermano na Foskolo walikuwa maaskofu wa Kanisa Katoliki katika Afrika Kaskazini ambao kwa kutetea imani sahihi waliteswa kikatili sana na Wavandali katika karne ya 5, wakati wa utawala wa mfalme Huneriki aliyekuwa Mwario. Hatimaye walipelekwa uhamishoni[1].

Habari zao zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita.

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 6 Septemba pamoja na Leto wa Nefta, askofu katika Tunisia ya leo, mtu shujaa na mwenye elimu kubwa, ambaye baada ya kufungwa muda mrefu katika hali ya kutisha alichomwa moto ili kuwatisha wenzake hao [2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.