Don Gordon (Mwigizaji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Don Gordon (wakati mwingine, huorodheshwa kama Donald Gordon kutokana na jina kamili: Donald Walter Guadagno; alizaliwa Los Angeles, California, 13 Novemba 1926 - 24 Aprili 2017) alikuwa mwigizaji wa filamu na vipindi vya televisheni wa Marekani.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Filamu zake maarufu ni zile alizoigiza akiwa na mwenzake Steve McQueen hasa Bullitt, Papillon na The Towering Inferno. Aliigiza kama mwigizaji mgeni katika kipindi cha McQueen katika stesheni ya CBS kilichoitwa Wanted: Dead or Alive. Katika mwaka wa 1981, Gordon aliigiza kama msaidizi wa Mpinga Kristo Damien Thorn katika filamu. Gordon ,pia, aliigiza sehemu ndogo kama afisa wa polisi katika filamu ya Lethal Weapon, iliyohusisha Mel Gibson na Danny Glover. Katika mwaka wa 1962, alichaguliwa kama mshindani kwa tuzo ya Primetime Emmy kwa uigizaji wake kama Joey Tassil katika kipindi cha CBS cha The Defenders.

Gordon aliigiza katika toleo la In a Deadly Fashion la 1959 katika kipindi cha televisheni ya Border Patrol, kilichohusisha Richard Webb. Uigizaji mwingine wa Gordon ulikuwa katika toleo la kipindi cha Twilight Zone lililoitwa The Four of Us are Dying. Katika msimu wa 1960 -1961, Gordon alikuwa mwanachama katika kipindi cha The Blue Angels akiwa pamoja na waigizaji maarufu kama Dennis Cross, Warner Jones, Morgan Jones, na Mike Galloway. Kipindi hicho kilikuwa kama makumbusho ya kikundi maarufu cha rubani mashuhuri wa kivita wa Marekani kilichoitwa Blue Angels (Malaika Samawati).

Mwaka wa 1963, Gordon alihusishwa katika "Without Wheat, There is No Bread katika kipindi cha CBS cha The Lloyd Bridges Show. Mwaka uo huo, yeye alihusishwa katika kipindi cha televisheni ya stesheni ya NBC cha The Eleventh Hour. Katika msimu wa 1963 -1964, yeye aliigiza kama askari kutoka vita ya Vietnam Kusini katika kipindi cha ABC, Channing ,kilichohusisha kampasi ya kubuni ya Chuo cha Channing.Channing ilihusisha waigizaji maarufu kama Jason Evers na Henry Jones. Alipewa jukumu jingine katika toleo la The Invisible katika kipindi cha The Outer Limits. Katika mwaka wa 1974, yeye aliigiza mhusika ambaye ni mwasi aliyekuwa ametoka gerezani. Mhusika huyu anauawa na Dick Van Dyke katika toleo la kipindi cha Columbo la Negative Reaction.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]