Don Cartagena ni jina la kutaja albamu ya tatu ya msanii wa muziki wa hip hopFat Joe. Hii ni albamu yake ya kwanza tangu kuingia mkataba na studio ya Atlantic Records. Vilevile ni albamu yake ya kwanza kushirikisha wasanii wa hip hop mchanganyiko. Wasanii hao ni pamoja na Nas, Big Pun, Jadakiss, Raekwon, Terror Squad, Diddy, na Layzie Bone. Don Cartagena iliingia nafasi ya #7 kwenye chati za Billboard 200 ikiwa na mauzo ya nakala 40,000. Albamu ilitunukiwa Dhahabu kwa mauzo ya nakala takriban 500,000 huko nchini Marekani.