Nenda kwa yaliyomo

Don Cartagena (wimbo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Don Cartagena”
“Don Cartagena” cover
Single ya Fat Joe na Diddy
kutoka katika albamu ya Don Cartagena
Imetolewa 1 Septemba 1998
Muundo CD single
Imerekodiwa 1998
Aina Latin hip hop, gangsta rap
Studio Atlantic Records
Mtunzi J. Cartagena
Mtayarishaji Richard "Younglord" Frierson
Mwenendo wa single za Fat Joe na Diddy
"Envy"
(1995)
"Don Cartagena"
(1998)
Bet Ya Man Can't (Triz)
(1998)

"Don Cartagena" ni wimbo kutoka katika albamu ya Fat Joe ya Don Cartagena. Wimbo umeshirikisha P. Diddy kwenye upande wa kiitikio, ambaye humu kaimba kiitikio tu (lakini pia hakuonekana ndani yake video yake). Wimbo umetayarishwa na mtayarishaji machachari - Younglord. Wimbo umebahatika kushika nafasi ya #21 kwenye chati za Hot Rap Singles na nafasi ya #40 kwenye chati za Hot R&B/Hip-Hop Singles & Tracks.

Muziki wa video

[hariri | hariri chanzo]

Muziki wa video wa wimbo huu unaanza na watoto wengi wakiendesha baiskeli barabarani huku ikioneshwa matairi ya baiskeli yanageuka kuwa matairi ya gari. Wakati huohuo anasikika Fat Joe akizingumzia habari za utotoni mwake jinsi walivyoweza kuanzisha kijikikundi kidogo cha shule - pia akihadithia kwamba walikuwa na baba yao aliokuwa akisadia kwa kila walichokitaka, lakini pia kulikuwa na njemba moja aliyeitwa Santiago alikuwa akiogopeka sana. Kwani ukimuona huyo bwana, basi ujue maisha si mazuri tena. Baadaye Fat anaonekana kurudisha kisasi kwa yule bwana Santiago na kupewa heshima kubwa kwa marafiki zake waliokuwa wakihofia mtandao wa Santiago. Pichani, anaonekana mfuasi mmoja mmoja anauawa wa Santiago - na mwishowe yeye mwenyewe Santiago.

Chati Nafasi
Hot Rap Singles # 21
Hot R&B/Hip-Hop Singles & Tracks # 40

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]