Nenda kwa yaliyomo

Desideri wa Langres

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kifodini cha Mt. Desideri.

Desideri wa Langres (alizaliwa Genova, Italia; alifariki karibu na Langres, Ufaransa, 355) alikuwa askofu wa 3 wa mji huo.

Atanasi wa Aleksandria alimtaja kati ya walioshiriki Mtaguso wa Sardica (343).

Aliuawa na mfalme wa Wavandali kwa kukatwa kichwa mara alipokwenda kwake kutetea wananchi dhidi ya wavamizi hao, naye alikubali kwa utulivu kuwafia kondoo zake [1].

Hata hivyo pengine wamechanganywa maaskofu wawili wa Langres wenye jina hilohilo moja, ambaye wa pili aliuawa mwaka 407.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Mei[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.