Dayolojia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kitabu cha Galileo Galilei kinachoitwa Dayolojia kuhusu namba mbili za kuelewa ulimwengu, 1632.

Dayolojia (kwa Kiingereza: "dialogue" na pia "dialog"[1], kutoka maneno ya Kigiriki διά, dia, kati ya na λόγος, logos, neno[2]) ni mazungumzo ya kupokezana kati ya watu wawili au zaidi.

Dayolojia huweza kuwa ya ana kwa ana baina ya wazungumzaji au kwa njia ya simu, maandishi n.k.

Dayolojia ya ana kwa ana ni mazungumzo ya kupokezana baina ya watu ambao huonana.

Dayolojia inaweza kubuniwa pia. Hapo mtunzi hana budi kujifanya kama mhusika katika dayolojia hiyo.

Katika kutunga dayalojia mtunzi hana budi kujifanya kama mhusika katika dayalojia hiyo. Kwanza anapaswa kutafakari kwa makini mada anayokusudia kuandikia dayalojia, kutayarisha na kupanga mawazo kimantiki na kwa mtiririko na kufikiria wahusika na kuwapangia majukumu kulingana na matendo yao. Kwa mfano kama mhusika ni mkulima, lugha anayopewa, vifaa anavyosemekana kuvitumia na mandhari aliyomo ni lazima vifanane na hali ya mkulima halisi.

Mambo ya kuzingatia katika dayalojia ni pamoja na haya yafuatayo:

  1. Kutoa maelezo ya ufafanuzi katika mabano ili kumfahamisha
  2. Kuwa na mazungumzo ya mkato na yasiyozidiana sana kati ya wahusika. Mhusika mmoja asitawale mazungumzo kupita wengine.
  3. Kutumia vihisishi ili kufanya dayalojia iwe ya kusisimua
  4. Pawepo mwingiliano wa mazungumzo ya wahusika na kudakia maneno ili dayalojia iwe na uhalisia.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Dialogue", Oxford English Dictionary, 2nd edition
  2. Jazdzewska, K. (1 June 2015). "From Dialogos to Dialogue: The Use of the Term from Plato to the Second Century CE". Greek, Roman and Byzantine Studies 54.1 (2014), p. 17-36. 
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dayolojia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.