Nenda kwa yaliyomo

Dambudzo Marechera

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dambudzo Marechera (4 Juni 1952 - 18 Agosti 1987) alikuwa mwandishi wa riwaya, hadithi fupi, michezo na mashairi wa Zimbabwe. Alijulikana sana kwa maandishi yake ingawa alifukuzwa katika vyuo vikuu kwa sababu ya tabia yake mbaya, licha ya kufaulu katika masomo yake.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Marechera, kwa jina la Kikristo aliiitwa Charles William, alizaliwa katika mji wa Vengere, Rusape, nchini Rhodesia Kusini, kwa Isaac Marechera, mhudumu wa chumba cha kuhifadhi maiti, na msichana Masvotwa Venenzia Marechera aliyekuwa mtoto wa wazazi Washona kutoka sehemu ya mashariki-kati ya Rhodesia.

Katika kitabu chake cha mwaka 1978 kinachojulikana kwa jina la The House of Hunger, na katika mahojiano, Marechera mara nyingi alidanganya kuwa baba yake aliendesha "treni ya karne ya 20" au "alirudi nyumbani na kisu kikiwa kimemchoma kwa nyuma" au "alipatikana katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali na mwili wake ukiwa umejaa risasi". Udanganyifu huo ulimpelekea Marechera kudanganya hata juu ya "ukweli" wa maisha yake mwenyewe. Mnamo Aprili mwaka 2021, mtafiti wa Ujerumani Flora Veit-Wild alitoa ufafanuzi mkubwa kuhusu kaka wa Marechera, Michael, juu ya jambo la uharibifu katika maisha ya Marechera, mdogo wake. Michael alisema kuwa Dambudzo alikuwa mwathiriwa wa mama yao muti, akimaanisha kwamba alilaaniwa kwa namna  fulani kwani Marechera aliporudi kutoka London kuwa mwandishi wa makazi katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe, mama yake na dada zake walijaribu kuja kumlaki lakini aliwakataa kwa mkono wake mwenyewe, akimshtaki mama huyo kwa kujaribu kumuua. Bado, inajulikana kwamba Marechera hakuwahi kufanya bidii kukutana na mtu yeyote wa familia yake kabla ya kufariki mwaka 1987.

Bibliografia

[hariri | hariri chanzo]
  • 1978: The House of Hunger
  • 1980: Black Sunlight
  • 1984: Mindblast or The Definitive Buddy
  • 1992: The Black Insider
  • 1992: Cemetery of Mind
  • 1994: Scrapiron Blues

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]