Beseni la Columbia
Beseni la Columbia (kwa Kiingereza: Columbia Plateau au Columbia Basin) ni eneo maalum la kijiolojia na kijiografia kaskazini-magharibi mwa Marekani, likiwa katika majimbo ya Marekani ya Washington, Oregon, na Idaho. Ni eneo kubwa lililotokana na mkondo wa mwamba wa gumawesi (basalt) ulioenea kati ya milima ya Cascades na Milima ya Rocky Mountains katika kipindi cha milipuko ya volkeno iliyopandisha magma kutoka koti la Dunia ambayo iliganda kwenye uso wa ardhi. Mto Columbia unatiririka katika eneo hilo.
Jiolojia
[hariri | hariri chanzo]Takriban miaka milioni 16 hadi 5 iliyopita volkeno zilimwaga kutoka chini kiasi kikubwa cha lava kilichoenea katika kilomita za mraba 160,000 na kuganda kwa unene wa kilomita 1.8.[1]
Wakati mwamba kiowevu ulipanda juu, uso wa ardhi ulishuka polepole katika nafasi iliyotokea chini yake.
Kwa njia hiyo lilitokea beseni la mto Columbia lenye miinuko kati ya mita 60 hadi 1,500 juu ya u.b.[1]
Tabianchi na uoto
[hariri | hariri chanzo]Tabianchi ni nusu yabisi na uoto asilia ni hasa vichaka na nyasi [2].
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Miji ya jimbo la Washington katika Beseni la Colombia ni pamoja na:
Miji ya Jimbo la Oregon katika Beseni la Columbia ni pamoja na:
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "Description: Columbia Plateau Columbia River Basalt". United States Geological Survey. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-11. Iliwekwa mnamo 2007-10-09.
- ↑ https://www.britannica.com/place/Columbia-Plateau
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Ukurasa wa USGS kwenye Columbia Plateau Ilihifadhiwa 4 Desemba 2013 kwenye Wayback Machine.
- Jiografia ya eneo la Burudani la Ziwa la Roosevelt (chanzo cha ukurasa mwingi)
- Mwongozo wa hati na picha za dijiti kuhusu eneo la Mto wa Columbia.
- Jalada la Historia ya Kikabila cha River River
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Beseni la Columbia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |