Nenda kwa yaliyomo

La Paz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Chuqi Yapu)
La Paz

Kitovu cha mji wa La Paz
Habari za kimsingi
Utawala Mkoa wa La Paz
Historia ilieundwa 20 Oktoba 1548 kwa jina "Nuestra Señora de La Paz"
Anwani ya kijiografia Latitudo: 16°29′39"S
Longitudo: 68°8′51"W
Kimo 3,650 m juu ya UB
Eneo 255 km² (rundiko la mji)
Wakazi - mji: 835,167 (2006)
- rundiko la mji milioni 1.6
Msongamano wa watu watu 6,275 kwa km²
Simu +591 (nchi) 2 (mji)
Mahali

La Paz (pia: Chuqi Yapu) ni mji mkubwa katika nyanda za juu za Bolivia na makao ya serikali na bunge. Hali halisi ni mji mkuu wa nchi hata kama katiba imetaja Sucre kama mji mkuu.

Mji uko kwenye kimo cha mita 3,600 juu ya UB katika bonde la mto Chokeyapu linalohifadhi mji dhidi ya upepo na baridi. Kando ya La Paz umekua mji jirani wa El Alto kwenye tambarare ya juu mahali pasipo hifadhi. El Alto iko m 1000 juu ya La Paz na hapa wamekalia watu maskini katika hali ya hewa ambayo ni baridi zaidi.

Mlima Illimani wenye m 6,462 unasimama juu ya miji miwili ya jirani.

Tangu mwaka 1898 La Paz imekuwa mji mkuu hali halisi.

Picha za La Paz

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Bolivia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu La Paz kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.