Nenda kwa yaliyomo

Bustani za Forodhani, Zanzibar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bustani za Forodhani kama zinavyoonekana kutoka kwenye ukumbi wa mbele wa Jumba la Maajabu (House of Wonders).
Kando ya pwani katika Mji Mkongwe, Zanzibar, gazebo ya jiwe iliyofufuliwa hivi karibuni katika Bustani za Forodhani.
Wapishi wakionyesha vyakula vinavyouzwa katika bustani, Bahari Hindi ikionekana kwa nyuma.

Bustani za Forodhani (pia hujulikana kwa Kiingereza kama Forodhani Gardens, Jubilee Gardens na zaidi hivi karibuni kama Forodhani Park)[1] ni bustani ndogo kwenye Mji Mkongwe wa Zanzibar, Tanzania.

Bustani hizo ziko kando ya mtaa wa Mizingani unaopita ukingo wa bahari wa Mji Mkongwe, mbele tu ya majengo ya Jumba la Maajabu (House of Wonders) na Ngome Kongwe (Old Fort). Bustani hiyo ilianzishwa mwaka 1936 na kufunguliwa rasmi tarehe 21 Desemba 1936 kwa maadhimisho ya jubilii ya miaka 25 za utawala wa Sultani Khalifa bin Harub wa Zanzibar (silver jubilee) na pia kwa heshima ya marehemu mfalme George V wa Uingereza aliyewahi kutimiza miaka 25 ya utawala kwenye mwaka 1935[2]. Ilijulikana kama Jubilee Gardens ikabadilshwa jina baada ya mapinduzi ya Zanzibar ya 1964[3].

Shughuli katika bustani

[hariri | hariri chanzo]

Bustani zina shughuli nyingi haswa baada ya jua kuchwa, wakati watalii na wenyeji vilevile hukusanyika kwenye soko maarufu la barabara la chakula katika uwanja mkuu, kula chakula cha jioni wakifurahia vyakula vitamu vya Waswahili na Wazanzibar kama vile dagaa wa baharini, samamo, mihogo na viazi vitamu.[4] Mnamo 31 Julai 2009, hafla ya kuvunja ardhi ilifanywa na Aga Khan kuanzisha bustani iliyofufuliwa. Ilirekebishwa na Agha Khan Trust for Culture (AKTC) kwa gharama ya $ milioni 3 (Shilingi bilioni 3.9) kutoka kwa makadirio ya awali ya $ milioni 2.4 (zaidi ya Shilingi bilioni 3).

Ukarabati huo wa juu ulihusisha urejeshwaji wa barabara za waenda kwa miguu, mandhari, uboreshaji wa miundombinu, ikijumuisha taa, mifereji ya taka na vifaa vya uraia, na ukarabati wa ukuta wa bahari ulio mbele ya bustani.[5]