Nenda kwa yaliyomo

Kombe-kikonyo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Brachiopoda)
Kombe-kikonyo
Mfano wa kombe-kikonyo (Lingula anatina)
Mfano wa kombe-kikonyo (Lingula anatina)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
Faila ya juu: Lophotrochozoa
Faila: Brachiopoda
Duméril, 1806
Ngazi za chini

Nusufaila 3, ngeli 3:

Kombe-kikonyo ni wanyama wa bahari wa faila Brachiopoda walio na makombe mawili, moja mgongoni na moja tumboni, na kikonyo kinachotumika kujiambatisha kwenye uso wa chini. Katika kombejozi kila kombe liko kwa ubavu. Makundi fulani ya kombe-kikonyo, kama vile familia Craniidae, hayana kikonyo na hujiambatisha mara kwa mara kwa uso wa chini.

Umbo la makombe na kazi yao

[hariri | hariri chanzo]
Kombe-kikonyo wenye kifundo:
Kijivu iliyoiva - Kombe la kikonyo
Kijivu iliyofifia - Kombe la mikono
Pinki – Kikonyo
Kijani nyeusi - Uso wa chini

Urefu wa kombe-kikonyo wa kisasa ni mm 1-400, lakini spishi nyingi ni karibu mm 10-30[1]. Magellania venosa ndiyo spishi kubwa kabisa iliyopo yenye upeo wa sm 40[2]. Kombe-kikonyo wana makombe mawili ambayo hufunika pande za juu na chini za mnyama, tofauti na moluska wa kombejozi ambao makombe yao hufunika nyuso za mbavu. Makombe hayo hayana usawa katika saizi na muundo, na kila moja lina umbo lake la ulinganifu badala ya haya mawili kuwa maono ya kioo ya kila moja.

Kombe la mikono kwa kawaida ni dogo zaidi na hubeba mikono (brachia) kwenye uso wake wa ndani. Mikono hiyo (au brachia) ndiyo asili ya jina la faila na zinabeba lofofori (w:lophophore) inayotumiwa kwa kujilisha kwa kuchuja na kupumua. Kombe la kikonyo kwa kawaida ni kubwa zaidi na lina mwanya karibu na bawaba unaowezesha kikonyo kinachofanana na bua kipitie. Kombe-kikonyo wengi hukitumia kujishikamanisha kwenye uso wa chini[3]. Makombe ya mikono na ya kikonyo mara nyingi huitwa kombe la juu au la mgongo na kombe la chini au la tumbo, mtawalia. Kombe la tumbo liko juu ya kombe la mgongo wakati spishi nyingi za wanyama hawa wameelekezwa katika mkao wa maisha. Kwa kawaida makombe ya kombe-kikonyo wenye kifundo ni mbenuko yote mawili na uso wao mara nyingi huwa na mistari ya ukuaji na/au mapambo mengine. Walakini, Lingulida, ambao hawana kifundo na kuchimba ndani ya sakafu ya bahari, wana makombe yaliyo laini na bapa zaidi na ya ukubwa na umbo sawa[3].

Kombe-kikonyo wenye kifundo (Kiing. articulate) wana mpangilio wa jino na soketi ambao makombe hutumia kwa kujifunga na kujifungua, na huzuia makombe dhidi ya miwendo ya upandeupande. Kombe-kikonyo bila kifundo (Kiing. inarticulate) hawana meno na soketi zinazofanana. Makombe yao yanashikiliwa pamoja na misuli tu. [3]

Kombe-kikonyo wote wana misuli nywezi iliyomo ndani ya kombe la kikonyo na ambayo hufunga makombe kwa kuvuta sehemu ya kombe la mkono mbele ya bawaba. Misuli hiyo ina nyuzi "haraka" ambazo hufunga makombe wakati wa dharura na nyuzi za "kushika" ambazo ni polepole lakini zinaweza kuweka makombe yakifungika kwa muda mrefu. Kombe-kikonyo wenye kifundo hufungua makombe kwa kutumia misuli tanuzi iliyomo zaidi kwa nyuma na kuvuta sehemu ya kombe la mikono nyuma ya bawaba. Kombe-kikonyo bila kifundo hutumia mbinu tofauti wa ufunguzi ambao misuli hutumia kupunguza urefu wa uwazi mkuu wa mwili na kumfanya ubenue nje na kutanua makombe. Makundi yote mawili hufungua makombe mpaka pembe ya takriban 10°. Seti tata zaidi ya misuli inayotumiwa na kombe-kikonyo bila kifundo pia inaweza kutumia makombe kama mkasi, mbinu ambao Lingulida hutumia kuchimba[4].

  1. Cohen, B.L (2006). "Brachiopoda". Encyclopedia of Life Sciences. John Wiley & Sons, Ltd. ISBN 978-0470016176.
  2. Rediscovery of Terebratulina austroamericana Zezina, 1981 (Brachiopoda: Cancellothyrididae) from off northern Chile
  3. 3.0 3.1 3.2 Moore, R.C. (1965). Brachiopoda. Treatise on Invertebrate Paleontology. Juz. la Part H., Volume I. Boulder, Colorado/Lawrence, Kansas: Geological Society of America/University of Kansas Press. ku. H440. ISBN 978-0-8137-3015-8.
  4. Ruppert, E.E; Fox, R.S.; Barnes, R.D (2004). Invertebrate Zoology (7 ed.). Brooks / Cole. ISBN 978-0-03-025982-1