Borja Mayoral

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Borja Mayoral

Borja Mayoral Moya (alizaliwa tarehe 5 Aprili 1997) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Hispania ambaye anacheza kama mshambuliaji katika timu ya klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Hispania.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Borja Mayoral alizaliwa huko Parla, Madrid. Mayoral alijiunga na vijana wa timu ya Real Madrid mwaka 2007.

Mwaka 2014, alijumuishwa katika kikosi A cha Juvenil, na pia alifunga magoli saba katika Ligi ya Vijana ya UEFA, ikiwa ni pamoja na magoli matatu(Hat-trick) katika ushindi wa kikundi cha PFC Ludogorets Razgrad.

Tarehe 2 Machi 2016, kutokana na kuumia kwa Karim Benzema, meneja Zinedine Zidane alimpa Borja Mayoral nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza katika mechi ya Real Madrid dhidi ya Levante UD. Siku ya mwisho ya msimu wa akiba, alifunga mara mbili kwa ushindi wa 6-1 dhidi ya La Roda CF.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Borja Mayoral kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.