Boeing 747

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Boeing 747 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini München mnamo tarehe 15 Februari, 2015.

Boeing 747 ni ndege ya kampuni ya Marekani iitwayo Boeing yenye upana mkubwa kwa ajili ya kubebea mizigo au kusafirishia abiria.

Pia ndege hii inajulikana kwa jina la "Jumbo jet", Ndege hii ni moja ya ndege ambazo inajulikana sana Duniani na ndo ilikuwa ndege ya kwanza kutengenezwa ikiwa na umbile pana katika ndege zote zilizo tengenezwa na kampuni hii. Hii ni ndege yenye injini nne.